Advancing

Uvundo

Mjini sijakuja kutafuta kazi
Kutafuta pesa na uhali
Kutafuta maisha mema
Kutafuta kuishi nitafune

Kama kazi mashambani ipo
Uzembe na tamaa tu
Kutaka vya haraka nenesha
Jasho ya nini kama vipo

Kila uchao kuamka
Kuamka kwenda kazini
Kumfanyia muajiri kazi
Kazi isoisha na kukitiri

Utumwa iliyoje kama
Kutunukiwa ni kwa hiari
Hiari ya mwajiri aso’utu
Utu ni ndoto ilo’fikirani

Kila mara ni ahadi tu
Ahadi tupu ziso’kweli
Maanake kukuweka na tarajio
Fala tu ano’ishi kwa ahadi

Matarajio hayaliwi hayalambwi
Alo na njaa hasira imemjaa
Kukiuka kuua kuvunja kuzini
Ndoto ya wema inamweka

Kupakwa mafuta mgongoni
Kupumbaza kunajisi uhali
Mtazamo haufuti ufukara
Bidii jasho umahiri ukombozi

Standard