Advancing

Kama nipo, naishi au la?

Nywele kavu halafu
Uso chapwa ulokauka
Hauna hisia yeyote
Macho yanaona vimulimuli

Ngozi imekauka ikakauka
Pua halinusi chochote
Kama Tundu ardhini
Kuwepo bila matumizi

Midomo kinywa meno
Vidole vya mikono
Vidole vya miguu
Kifua mapaja misuli

Kufikia nyayoni kujigundua
Sauti ipo inakohoa
Nipo? Nipo labda
Uteshi wa kimawazo

Advertisements
Standard
Advancing

US Marshals is auctioning 50,000 Bitcoins Seized from Ross Ulbricht

The U.S. Marshals Service will auction off another 50,000 bitcoins that were seized from a computer belonging to Ross Ulbricht, the alleged owner of the online black-market bazaar, Silk Road.

The auction scheduled to be held on December 4th, and will only be open to pre-registered bidders. According to Coindesk, the agency will begin accepting bids starting today, and ending on December 1st.

Over two rounds, the Marshals Service will auction off 10 blocks of 2,000 BTC in the first round followed by 10 blocks of 3,000 BTC in the second. Participants will also need to make initial deposits of $100,000 and $150,000 for the two rounds. The winner will be notified on December 5th, and payment is due by the 8th.

With bitcoins worth around $400 currently, the value of coins are at roughly $20 million, Coindesk calculates.

Standard
Advancing

Chakaramu

Kuna watu wanaonunua heshima kwa roho zao. Baadhi kwa fedha na utajiri wao. Wachache kwa yote mawili. Wengi huuza heshima zao kwa fedha! Na wengi zaidi, heshima zao huuzwa bila ya wao wenyewe kutambua. Aaaaa…ukweli jinsi ulivyo. Ukweli kwamba kila mtu ana nia ya kuishi. Kila mtu anataka kuishi vyema kama mtu yeyote yule. Ndiyo nguzo ya kuwepo. — Said A. Mohamed

Standard
Advancing

Utupu

Mvuto wa usasabaadaye
Ati wanacheka tu
Hata sisi wenyewe tunacheka
Tunachekana…uyeye..umimi..utupu!

Mtu aliyepoteza imani
Na kila kitu
Iweje aweze kutabiri nafuu?
Ukweli wa uwongo…utupu!

Pengo..kutofahamu
Mizizi ya tamaa
Kung’ang’ania mfululizo
Msito..nafsi tupu!

Kutofikiri kutotazamia
Kutozingatia mambo vizuri
Kuzuia fikira na lawama
Yayo kwa yayo…utupu!

Pengo…pengo jingine
Mtu huitafuta vipi baadaye
Yake katika dunia ya leo?
Choyo na kuchukiana…utupu!

Standard