Advancing

Tamaa

Mabadiliko
Mashiko
Msikitiko
Kuna ukomo?

Vumbi kuvumbishwa
Tope kupakwishwa
Damu kuloweshwa
Donda kutoneshwa

Siasa
Elimu
Jamii
Dini
Utandawazi na upotevu

Jana haijulikani
Leo haipo tena
Kesho nayo si bayana
Tamaa na tamani

Uhuru tunao?
Wa ndugu kumtesa ndugu
Kung’ang’ania na kupora jamii
Kujilimbikizia mtaji
Huduma kwa jamii kukatiza
Kuelekeza vyote kwako
Wenzako wakilamba vumbi
Na tope kujaribu kuishi
Maisha ya kukodesha

Maneno
Silaha
Na hadaa
Kila siku
Kila kitu kukoma

Tatizo si rangi
Tatizo si kabila
Tatizo si ukosefu
Tatizo ni tamaa
Midomo wazi
Nyuso zi’so haya wala huruma
Tamaa!

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s