Nilipofariki dunia
Nilipokata pumzi
Mawingu yalikuwa manyamavu
Kila kitu kilinikataa
Nilipoteza hisia
Sikukuwa na maana tena kwa vyovyote vile
Maisha niliyoishi yakuwa na maana tena
Nilibakia tu kama bofu lililotolewa hewa
Marafiki waliendelea na maisha yao
Ingawa walihuzunika kunipoteza
Iliwachukuwa siku chache kunisahau
Shughuli za kawaida hazikukatizwa
Ndege wa angani waliendelea kuimba
Jua liliangaa kama kawaida
Mito iliendelea kutiririka
Mimea iliendelea kukua
Wapendwa wangu walihuzunika
Walilia zao kwikwi
Macho yakabadili rangi
Yakawa mekundu
Huzuni ulitanda
Walijua huo ndio ulikuwa mwisho wa kuniona
Pindi tu niingiapo kaburini
Watamkosa mmoja wao wa hali na mali
Wao tu ndio walioadhirika
Maisha ni mafupi
Yale uyapitiayo leo
Ni muhimu kukukuza kwa minajili
Ya maisha ya kesho na baadaye
Makosa ya sasa na yawe funzo
Ili kujiendeleza
Aliyeteleza na kuanguka na kusimama
Yu imara kuliko yule
Alibaki imara bila ya kuteleza
Nilipozikwa niliwaacha waja wenzangu
Wakiendelea kubahatisha maisha
Bila ya kujua kuwa hata wao
Siku moja wataiwacha dunia
Waliendeleza dhuluma zao za kila siku
Mabaya kutendeana na kuwakera wengine
Maisha ni mafupi
Kila kitu kina mwisho wake
Hakuna jambo lisilo na kikomo
Vilio na huzuni vitapoa
Upendo utabaki
Tuukuze upendo zaidi na zaidi
Ili kujiepusha na majanga ya kujitakia
Kama wanadamu
Tusiishi maisha ya kinyama
Tuishi kwa amani na upendo
Tuhubiri umoja wa jamii