Advancing

Hawatuelewi

Moja wapo ya zile fikra
Ambazo huwa zimebanwa
Na kunyimwa hata pengo
La kutokezea waziwazi!

Hawatujui na hawatatujua kamwe
Hawatufahamu
Maisha yetu
Vilio vyetu
Pande zote
Mauwaji na majonzi
Harakati kujaribu kujituliza
Fununu tu za kimaumbile

Majaribio ya kimwili
Tamaa na utelezi
Cha mwenzio kuonekana tamu
Chako kukosa hamu
Kuitumia kila njia
Kuonja vya kila pande
Maadamu kutuliza hamu
Hamu isiyo na Mwanzo wala mwisho
Karne zimepita
Hakuna aliyefanikiwa
Kuituliza hiyo hamu
Itakuwa hata baada ya sisi
Kuuwacha ulimwengu huu

Hii ni ya wangu wa moyoni
Wangu warembo wawili
Jasho kunitoka
Ili kujikimu
Kupata kidogo
Ingawa cha maana
Kuendeleza maisha
Penzi langu litadumu
Hata ikiwepo mihemko
Na mawimbi au visiki
Mimi nipo hadi mwisho

Kwa marafiki na walimwengu
Hasa wale wa karibu sana nami
Maadui na wenye uhasama dhidi yangu
Niliyo jaliwa na Maulana
Hamuwezi kuninyang’anya
Nipo basi
Hata bila ya kutarajiwa

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s