Advancing

Labda

Ama tuseme tumenawiri. Ndio tumenawiri. Kivipi labda ndio italeta utata. Tusijiulize wala tusijitie mashakani na wale walio ushukani kwa kupeleleza vipi tumenawiri. Tukubaliane tu kuwa tumenawiri. Na pia tunaendelea zaidi ya hapa tulipo. Hivi karibuni, tuseme zaidi ya karne moja, labda tutayaona na kukubaliana nao kuwa tumenawiri.

Miundo msingi ya kila sehemu ya uchumi wetu haipo tena. Tumekwama katika dunia ya kuwaza na kuota yale ya kale…kama kulikuwa na kale! Kale haikuwepo. Ni fikra tu za wale wanaodhania hapo awali kila kitu kilikuwa sawa zaidi na sasa. Kile tunachosahau ni kwamba nyakati zimebadilika. Mwongozo wa kufanya hili au lile umegeuzwa kwa namna nyingi mno. Kwa hii sababu, hatuwezi kulinganisha ya sasa na ya kale.

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s