Advancing

Hadi mwisho

Maisha ya sasa,
Tunaabudu na kuliwaza,
Lini maadili na ukakamavu,
Wa kila mtu utamfanya kunawiri,
Bila ya chuki au mabaya kuwafuata?

Naogopa mie maskini,
Hali yangu ya unyonge sijiwezi,
Elewa wazi kuwa sijimudu,
Pahala hapa pamejaa,
Upotovu, balaa na matanga,
Tujaribu kuepukana na kukopa,
Maisha tunayoishi ili tujimudu tuwezavyo.

Maswali ya ushupavu,
Mawili kati ya yote kumi,
Ni ya uovu,
Yote kwa ajili ya mvuto,
Mvuto wa kujifananisha,
Na wale walio na uwezo,
Uwezo kama sio unafiki,
Na dhulma za kimaisha.

Mtazame aliye chini yako,
Mtazame aliye juu yako,
Mtazame aliye katikati,
Katikati labda anapanda,
Labda anaporomoka,
Mwisho mtazame yule pale,
Aliyepitia haya yote,
Hata akaporomoka kwa ajili ya mvuto,
Mvuto wa majira ya usasa baadaye.

Mara kadha wa kadha,
Kila mja huwa ana nia,
Nia ya kujiendeleza,
Ingawa atagongwa,
Ama kuzuiwa na kukanyagwa,
Au kutemewa mate,
Yeye hujivuta ili kujikwamua,
Ili asiteremshwe chini zaidi na pale alipo.

Ama wakati mwingine,
Na sio kila mara,
Utapatana na waja,
Waliopata mvuto wa kujiinua,
Na kufika upeo wa juu kimaisha,
Na kudhibitisha kuwa bado kunao,
Mvuto wenye utu na maendeleo.

Tuungane na tuvutane,
Bega kwa bega,
Ili kijiinua kijamii,
Kuimarisha maisha ya sasa na kesho,
Kwani dunia hii sio yetu,
Ni mali ya kukomboa kwa wale wajao baada ya sisi kuondoka.

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s