Advancing

Hali yetu

Hivi ndivyo tulivyo. Undugu umetutoka. Hamna cha kaka wala dada. Tujuacho ni umimi na uwewe. Ingawa ni kweli kuwa kila mja alizaliwa pekee yake, mwanadamu ni kufaana. Nikune leo wayoni na kesho unapohitaji, nitakukuna mgongoni. Tuwache kuishi kana kwamba matatizo tul’o nayo hayatatutoka ikiwa hatutammaliza yule tumdhaniaye kuwa ni adui wetu.

Makabila ni mawili tu hapa tunapoishi. Tajiri na maskini. Au tuseme mtawala na mtawaliwa. Tunapowapatia watawala nguvu na mamlaka, wao hutugeuka na kutaka mamlaka na nguvu zaidi ili wabakie pale na kumkanyaga kabisa yule wanaomtawala ili asije kuropokwa au kukatizia starehe zao. Kuchovya mali ya umma na kulaghai ndio wajibu wao. Hata yule as’o na gari au mparapata anasukumwa kusaidia ujenzi wa barabara.

Advertisements
Standard

2 thoughts on “Hali yetu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s