Advancing

Hitaji…

Matarajio ya ubora,
Hamu ya usasa baadaye,
Bidii na uchovu,
Jasho la ukakamavu,
Yote kwa maana ya kufaulu,
Mwishowe kuondoka bila,
Dunia tu wasafiri tu!

Kwa hali ya kuishi,
Wakati mwingine,
Huwa kuna haja,
Ya mja anayekupa muda,
Zaidi nafsi yake,
Na hamu ya kuelewa,
Kujua yote yaendeleayo,
Mvutano wa nafsi yako,
Kukuelewa na kushiriki nawe,
Katika mazungumzo yako ya kindani,
Bila ya kujali lolote,
Wala kukushtumu,
Ama kukudhania vitofauti.

Msukumo wa aina yake,
Labda tu kimawazo,
Hutuepusha na ukweli,
Kutuchochea na kutukosanisha,
Na wale tuwaenzio kimaisha,
Kwa kutupatia hamu zisizo,
Hamu ya vile tudhaniavyo,
Kuwa ni tofauti na hiki au kile,
Njaa ya kimawazo,
Tamaa iso’ na dawa.

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s