Advancing

Kiwewe

Nilie na nani?
Vita,
Machozi,
Uchungu,
Masaibu,
Msambaratiko,
Huzuni kati ya mahaba,
Maporomoko na kuparamia,
Yote kwa kuwania uzuri na utu.

Ya juzi yalikuwa mema,
Badiliko likaja labda,
Uvumilivu ukakosa maana,
Tamaa ya yas’o maana kwangu,
Lawama zis’o mbele wala nyuma,
Kulimbikiziwa hasira na kero,
Utulivu kupepea,
Na kupaa kama tiyara,
Kisha kutokomea arijojo,
Ukavu ukaja na kilio.

Labda ni mimi,
Au pengine ni sisi,
Ama kweli ni wewe,
Ukweli haupo tena,
Kelele tu kila mara,
Mvua itakoma siku moja,
Unyevu kupotea,
Na unyamavu kurudi,
Pamoja na furaha,
Hilo ndio ombi langu.

Standard

Leave a comment