Advancing

Kuthubutu

Mtu hawezi kwenda mbele kwa kujali nafsi yake tu. Hataupata utulivu kwa sababu ya hatia ya kuipa mgongo jamii. Lazima mtu atazame kila upande. Kila sehemu, ili kukomesha kubomoka kwa maeneo yake. Kutilia maanani yaliyoharibika kama funzo na kukimbia kasi kutokana na tashwishi za kujimaliza ili kuimudu dunia ndiko kutaweza kumsukuma mbele pasi na hofu. Lazima mtu athubutu ndiposa afaulu. Hakuna njia ya mkato. Hakuna njia nyingine.

Utumwa wa wakati wetu. Utumwa kimya kimya. Utumwa wa kujipeleka mwenyewe sokoni kujiuza. Unajipata tu unafuata mwelekezo wa nguvu fulani kuendeleza matakwa yao. Unashurutishwa kwenda uchi ingawa wewe mwenyewe hutaki kwenda uchi. Unaharibu ya kwako kwa kutotaka. Hauna nguvu za kukataa. Unakwenda tu. Macho umefumba. Mwelekezi ni nafsi yako. Kufuata vivuli visivyo. Labda vipo. Labda ni hisia tu. Nafsi ya ndani kabisa kuilemea nafsi ya juu juu. Mvutano usiokuwa na mwisho. Dalili za uchakaramu labda!

Eti tunaambiwa dunia imekuwa ndogo. Imekuwa karibu. Teknologia na utandawazi umetufanikisha. Ufanisi kila sehemu ya jamii ya sasa. Lakini ufanisi ndio nini hasa? Kudhoofika kwa mila na tabia za kibinadamu, labda. Ama ni hali ya kuendeleza mipaka kati ya maskini na tajiri, na kufanikisha wachache?

Upungufu wa aina yake. Ndivyo maisha yalivyo. Mtu huzoeshwa vitu mpaka akavipenda kupita kiasi. Pale anapotaka kuwa navyo vitu hivyo, mara vyote hutoweka bila ya kutarajia. Maisha ndivyo yanavyokuwa labda, kuzoeshwa, kukimbiwa, kutamani na kukoseshwa.

Utulivu akilini. Hofu kutanda. Miale ya utanzu. Limbikizi za hamnazo. Mjazo wa hisia kali na maumivu kwa umbali. Njaa na hamu ya kila kitu. Hamu isiyoweza kutoshelezwa kwa vyovyote vile. Upungufu. Tamaa kutanda. Kuthubutu bila mafanikio. Hatma yake – kutwaliwa na kuzikwa!

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s