Advancing

Kuzama chini kabisa

Fikira za kiwazimu zilitanda na jasho jembamba kumtiririka. Ameshindwa aanzie wapi na amalizie wapi. Kumkosa mwenzi wake kumemkera mno. Hakutarajia yatampata ya leo akiwa hivi. Ni nini hasa kilimwingia akilini? Ama ni zile nguvu za kishetani? Amekuwa akilumbana na nguvu zisizoeleweka hivi karibuni. Yeye amekata shauri kuwa ni nguvu za kishetani hizo zinazomwandama siku hizi. Mbona alishikwa na mori kiasi hicho? Hangeweza kuielekeza nafsi yake isije ikakerwa kiasi hicho?

Aaah, potelea mbali! Hiyo ni ajali tu na hakutarajia atamwumiza wala kumuua huyo kijana. Kosa ni moja tu. Yeye na huyo msichana wamewahi kukwaruzana. Hiyo ilikuwa miaka michache hapo nyuma walipokuwa wakimfukuza mume mmoja. Ingawa hii ni ajali, dunia nzima itachukulia kuwa amemchoma kisu akiwa na haja ya kulipisha kisasi hicho cha miaka ya nyuma. Katika nafsi yake, yeye ana uhakika kuwa haya yote hayakupangwa na yametokea tu kighafla. Hana hatia yeye na hata hajawai kupania kumuumiza huyo dada, wala kumuua.

Alitazamia kujikwamua kutoka pale. Lakini alijipata tu anazama. Anazama zaidi na zaidi chini kwenye ardhi. Labda tuseme kwenye ardhi ya saba. Kule chini zaidi ya chini. Giza lilikoenea, kutambaa na kutawala. Vipi angejitoa mle gizani? Alijaribu kila awezalo kuukwea ukuta ili arejee kwenye mwangaza. Nguvu zilimwishia. Aliteleza kila alipojaribu. Akakwama na kukata tamaa. Mara fikra za kimweu zikamjia. Akawaza nazo. Aje iwe ni yeye tu anajikaza? Vipi itakuwa ikiwa atajivua nguo na kutembea huru? Huo ndio utakuwa mwanzo wake wa kujirehemu labda. Au labda avua kila kitu na kubaki mkavu alivyozaliwa! Ndiyo. Atajikomboa kutokana na utumwa wa kulazimishiwa mavazi. Hapo ndipo alikichukua kisu na kupasua mavazi yake yote. Akakusanya nguo zake zote na kuzitia moto. Akazichoma pamoja na nyumba yake. Alijiona amekombolewa. Alitabasamu. Kicheko kikamjia. Hata hajui kilitoka wapi. Kicheko cha chini kinachokaribisha. Kikafuatwa na kicheko cha wazimu kinachochosha. Akaaendelea kucheka. Akacheka bila kimomo. Hapo ndipo huyo dada alitokezea akamuonya kutochekacheka na kumwaribia yeye raha pale mtaani. Alijipata tu amekichomoa kisu na kumchoma mara kadhaa hadi akakata roho.

Hapo ndipo alizinduka na kujipata uchi huku kazungukwa na kundi kubwa la wapita njia. Alitumbukia tena katika lile shimo la giza na alipojitambua tena, alijipata katika hospitali ya kuwatibu wale waliosumbuliwa na akili. Kwake yeye aliita jela ya wendawazimu! Dunia imemwishia. Amefika kikomo chake.

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s