Advancing

Hitaji

Kukuwaza kila uchao,
U sehemu ya nafsi yangu,
Mahitaji yangu,
Tamanio langu,
Uponyo wa upweke wangu,
Ni wewe dawa yangu,
Uwa langu la moyoni,
Hurahisisha tamaa yangu,
Kunituliza kikamilifu.

Siku huwa refu,
Nikukosapo karibu,
Chakula sili,
Hewa hunikimbia,
Moyo husononeka,
Hadi ujapo,
Kunituliza tuli.

Raha naipata nikuonapo,
Karaha kwa mahasibu wetu,
Kufanya tuyapendayo,
Nafsi zetu kutulia,
Tamanio kutulizwa,
Kupepea mawazoni,
Hadi anga ya saba.

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s