Advancing

Kwa Umbali…

Najua unachotaka,
Usivuke mipaka,
Pole pole itafika,
Endelea kusaka,
Unapoenda kumekauka,
Haki yako utaipata,
Muda uta’po wadia.

Kilio chako,
Machozi yako,
Maumivu yako,
Mapuuza yako,
Siku itawadia kwako,
Utazawadiwa na kurambia,
Tamu kama sukari.

Fungua macho yako,
Usisifu tu kwa kusifu,
Hitaji ni lako,
Kwao sio hitaji,
Heri ujifiche,
Ujipange,
Ujijenge,
Lazima kujilisha,
Baadaye tupatane.

Nikumbatie,
Hamu imezidi,
Kukuona tu,
Malaika hunisimama,
Raha zako kwangu kuzidi,
Ndani ya roho kutulizwa.

Chuki ni uchafu wa moyo,
Usijitie hasara kwa chuki,
Kununa kwa watu ni kawaida,
Walimwengu wamejaa roho za kutu,
Kukupokonya vyako ndiyo raha yao.

Asiyekujua hatafahamu,
Wakati wako utafika,
Mafanikio yako,
Sio kipimo cha utu,
Maadui wanatambaa,
Kukutazama kila upande,
Kukucheka ukiporomoka,
Ubinadamu umewapotea.

Hakuna kitu kizuri,
Kama kuishi vyema,
Na watu wenzako,
Usichukie wenzio,
Usiwe na roho mbaya,
Atakaye kuzika humjui.

Tulia tuli,
Umewekwa ukawekeka,
Usiwe kiruka njia,
Na baadaye kumlaumu kila mtu,
Kabati lako liwe lako,
Usiligeuze la dhobi!

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s