Advancing

Uwe Wangu

Mwendo wako,
Unanivuta kwako,
Kicheko chako,
Kinanitia pako,
Busu lako,
Linanizindua uweko,
Uandaapo piko,
Zaidi ya muuza soko,
Umbo lako hunitia hamu,
Mduara akili hunizunguka,
Kila nitiapo macho yangu kwako,
Kwa madaha hupita,
Labda nitatazama tu,
Ukinipa hata kimawazo,
Sita hamu tena.

Mapenzi kitu kitamu,
Yamekuwa tangu mwanzo,
Hayeshi kamwe,
Labda kwa mmoja kuaga,
Al’o baki huendelea mbele,
Hata kupatana na penzi mbadala,
Ingawa ni tofauti,
Bado ni penzi,
Raha kumpa anayependwa,
Machozi na kuvunjwa roho,
Kuchezwa na kulaghai,
Hila aina yake,
Vigumu kuponesha,
Iwapo kidonda kitatoneshwa.

Kukutunza nitakutunza,
Kwa kila njia,
Nitafanya hima,
Ili upate utakacho,
Utulivu hadi moyoni,
Uzuri wako kuzawadiwa,
Umetunukiwa mpenzi!

Advertisements
Standard

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s