Advancing

Tulizo

Maisha kwetu mtihani
Usitamani cha mwenzio
Vuna ulipopanda
Mvua itakunyeshea nawe pia
Jua hawawezi kuliziba
Hata kwa maovu na fikra mbaya

Mungu yupo
Na ni mwaminifu kwa wote
Un’o hitaji ni imani kwake
Maisha yatambe

Advertisements
Standard
Advancing

A closer look

Taking a look at my life
I realize that there is no much left
I Need to go down on my knees
And say a prayer before I go
Back to chasing my dreams

Blind to the daily on-goings
My life is out of luck
Been treated as a punk
My anger is raised
I can’t live a normal life,
Fool!

Walking around
Smiles allover the face
Reminiscing the pain and joy
Of days gone by
Life will never be as it seems
Everyday praying for better
Until the day this life ends!

Standard
Advancing

Nitulizie…

Mafanikio yangu yanakutegemea wewe. Iwapo upweke utanizidi, ni wewe dawa yangu. Machozi na maumivu yangu, ni wewe tu unayeweza kunituliza. Mtazamo na mwenendo wako, ni utulivu kwa yangu hofu.

Nikumbatie. Nikumbatie watuone. Wajinyonge wakitaka. Ili wajue kuwa ni wewe wangu. Roho zao zichafuke. Wivu uwazidie. Kisha watulie kwa ugunduzi wa undani wa penzi letu!

Standard
Advancing

Ungalipo hapa…

Tamanio langu ni…

Ningependa nikuone,
Niwe karibu nawe,
Niseme nawe,
Nikutazame machoni.

Naumia kwa upweke,
Roho yangu inakuhitaji,
Lakini u mbali,
Mbali nami,
Hata mawazoni,
Umenipotelea.

Lini utafika,
Uje tuonane,
Unipunguzie tamaa,
Tamaa na hamu,
Hamu ya kukuona,
Hata mara moja,
Tu kwa miezi,
Moyo utaridhika.

Maumbile yako,
Raha kwa macho,
Tamaa kuzidi ovyo,
Hata kuona popo,
Mchana bila moto,
Nipe hata robo,
Pande la roho,
Na penzi lako!

Standard